MTINDO WA MAISHA

JINSI YA KUBORESHA URAFIKI

Kupata na kuanzisha urafiki ni rahisi ila kazi huja kwenye kuulinda na kuuboresha hasa katika mazingira ya mtu kuwa mfanyakazi na mwenye familia. Hapa kuna mbinu chache za kukuwezesha kuboresha urafiki kati yako na rafiki zako wanawake / wasichana wenzio.
1. Kuombeana
Omba kwa ajili ya rafiki zako kila mara na ikiwezekana kwa majina. Pia angalau mara moja kwa mwezi muweze kuomba pamoja hata kama mpo maeneo tofauti.
2. Wasiliana mara kwa mara
Waonyeshe marafiki zako kuwa unawapenda na kuwajali kwa kuwasiliana nao mara kwa mara japo kwa sms na kujua wanaendeleaje au tu kuwasalimu. Hii huboresha urafiki wenu na kuwaweka pamoja hata kama mnaishi mbali mbali au mmetingwa sana na shughuli za maisha.
3. Kuwa Mwangalifu
Usieneze maneno ya uongo juu ya rafiki yako wala usimwambie mtu mwingine mambo ambayo rafiki yako amekuamini na kukuambia kama msiri wake. Siku zote uwe mwenye maneno ya kusaidia na sio kuharibu wala kusingizia. Tunza siri za rafiki zako kwa gharama yoyote.
4. Onyesha Kujali
Mpongeze rafiki yako kwa moyo wa dhati pale anapofanya jambo jema au kufanikisha hatua fulani kubwa katika maisha yake. Pia uwe naye anapopitia magumu na kumsapoti kwa hali na mali, uwe tayari kuwa sikio lake pale anapokuhitaji.
5. Samehe na Omba msamaha
Pale unapomkosea rafiki yako uwe mwepesi kuomba msamaha na kukiri makosa yako, na vile vile uwe mwepesi kusamehe pale unapokosewa maana hakuna mtu mkamilifu. Uchungu, kiburi na kinyongo huvunja na kuharibu kabisa urafiki.
6. Imarisha uhusiano wako na Bwana Yesu
Kwa kufanya hivyo utazidi kuiona furaha ya kweli na utaweza kuwa na uwezo wa kukabiliana na lolote katika urafiki wenu.

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger