MUNGU ANATAKA AKUTOE KWENYE BONDE LA UVULI WA MAUTI.



ZAB 107:10 waliokaa katika giza la uvuli wa mauti, wamefungwa katika taabu na chuma.

ZAB 23:4 naam nijapopita kati ya Bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimboyako vyanifariji.


Kuna mwingine amekaa kwenye bonde la uvuli wa mauti na mwingine anapita.


NATAKA UFAHAMU UKWELI HUU
  1. palipo na kivuli kuna kitu halisi, hivyo palipo na uvuli wa mauti kuna mauti yenyewe.
  2. uvuli wa mauti ni roho kamili kabisa inayofanya kazi kwenye maisha ya watu.
  3. uvuli wa mauti unamaanisha taabu, ugumu wa maisha masumbufu yenye lengo la kumuangamiza mtu.
  4. ukweli huu uufahamu kuwa mtu yeyote lazima apite kwenye bonde la uvuli wa mauti cha msingi hapaswi kukaa kwenye bonde la uvuli wa mauti kama mahali pa kudumu.
  5. bonde la uvuli wa mauti haliepukiki ni kwa yeyote yule tajiri, maskini n.k
  6. bonde la uvuli wa mauti halitabiliki.
  7. kwenye bonde la uvuli wa mauti ni kwenye hofu unapoona hofu ujue sio roho ya Mungu.
  8. ni mahali pa giza.
  9. ni mahali pa kukatisha tamaa.
  10. ni mahali pa kukataliwa na watu.
JINSI YA KUTOKA KWENYE BONDE LA UVULI WA MAUTI
  1. Jisalimishe maisha yako yote kwa Yesu.
  2. tambua kwamba umeshambuliwa na roho ya bonde la uvuli wa mauti
  3. tangaza vita kali ili utoke katika hilo bonde.
  4. Funga uvuli na uruhusu Nuru na uhai katika roho yako na maisha yako.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger