Kama unajisikia kukata tamaa, kuvunjwa moyo, kukataliwa na kusalitiwa. CHUKUA HII


BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,
Ni wengi wanaonishambulia,
Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,
Hana wokovu huyu kwa Mungu.
Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, 
Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
Zaburi 3:1-3
LAKINI WEWE MUNGU!
Huenda Mfalme Daudi wakati anaandika zaburi hii
alikua anajisikia kukata tamaa, kuvunjwa moyo, kukataliwa na kusalitiwa.
Bado aliamua kutazama uzuri wa Mungu! KUMBUKA;
Leo unaweza ukawa unapitia ugumu kwenye mahusiano lakini Mungu atakusaidia utatoka hujadhurika ktk hilo, unaweza ukawa na hitaji ambalo linakuchosha akili lakini leo hii Mungu atakutimizia, madaktari wanaweza wakawa wamekwambia una ugonjwa usiotibika leo hii Mungu ni mponyaji wako!
Hapo ulipo mambo yanaweza yakawa yanaonekana hayawezekani lakini kwa Mungu yote yanawezekana.
Ukiwa na imani yenye mtazamo huu basi utaona mkono wa Mungu ukitenda kazi kwenye maisha yako na utaishi maisha ya ushindi ambayo alikuandalia.
BARIKIWA SANA!
Share this article :

+ comments + 1 comments

January 29, 2020 at 12:21 PM

fghfghfg

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger