USIOGOPE!!!!



 
kwa nini usiogope?

Ayu 3:25 maana jambo hilo nichalo hunipata, nalo unitialo hofu 
     hunijilia.
HOFU NI UTUMWA
Rum 8:15 kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba yaani Baba.
2 TIM1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
HOFU INA ADHABU
1 Yoh 4:18 katika pendo hamna hofu ; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
HOFU INA ADHABU MAAMUZI YOYOTE YANAYOAMULIWA KATIKA HOFU YANAGHARIMU.UKIKAA KATIKA HOFU UTAKUW UNATEKELEZA ADHABU.

KATAA HOFU
kataa hofu maana Mungu ameweka nguvu ndani yako huna sababu ya kuogopa maisha, kwamba watakuonaje usipofanikisha mpango ulioanzisha, hofu ya kuachika hivyo unatenda dhambi ili usiachike n.k .Yaliyokuwako yamekuwako hivyo uwezi kubadilisha kitu cha msingi jitiishe kwenye mikono ya Mungu ili uwe salama.


MAOMBI
1. Nakataa kuogopa kwa sababu Mungu hakunipa roho ya woga   bali ya nguvu, na ya upendo na ya moyo wa kiasi katika Jina Yesu.
2. nafunga Roho YA hofu kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
3. kila nguvu nyuma ya kila kitendo cha hofu maishani mwangu ipigwe kwa hasira ya Mungu.
4. kila kitu ninachokiogopa naamuru kisinijilie (kataa kisikutokee) sasa katika jina la Yesu.
kila nilichowahi kukiogopa hakitanitokea katika jina la Yesu.
 
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger