maharusi wafungia ndoa chini ya maji

 waswahili husema ukisitaajabu ya Mussa utaona ya firauni. Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .Bwawa hilo hutumiwa kutoa mafunzo ya kupiga mbizi katika kituo cha Fort William.Bi Dorota Bankowska mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi jana lakini akataka sana kufanya jambo la kipekee wanakoishi kama ishara ya kusherehekea harusi yao.

Bi harusi alivalia gauni nyeupe huku bwana harusi akivalia sketi ambayo huvaliwa na waskochi ijulikanao kama 'Kilt'.Maharusi hao waliungana na marafiki wao Ala Bankowska na Charlie Cran-Crombien chini ya maji hayo.Wote wanne walivalia vifaa vya kupigia mbizi pamoja na mavazi yao ya harusi.


Takriban wageni 100 walitazama harusi hio wakiwa nje

SOURCE: BBC
Share this article :

+ comments + 1 comments

June 11, 2020 at 8:22 AM

fggffg

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger