Taarifa ya (CAG) yakutwa ikisambazwa mitaani ikiwa imenyofolewa kurasa



.


Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa  hesabu za serikali  kuhusiana na kashfa ya wizi wa bilioni 321 kwenye akaunti ya tegeta Escrow iliyokabidhiwa kwa katibu wa bunge imekutwa inasambazwa mitaani huku ikiwa imenyofolewa kurasa tatu za mwisho zenye majina ya   waliohusika na mgawo wa fedha hizo kwa lengo la  kutengeneza propaganda ili kuwadanganya wananchi  kuwa taarifa hizo hazijawataja wahusika. 
Akizungumza na  waandishi wa habari mwenyekiti mwenza wa ukawa Mh. James Mbatia  amesema zipo taarifa za baadhi ya waliokuwa   wanasambaza taarifa hizo kuwa wamekamatwa na jeshi la polisi na kuwataka wananchi  kutoa taarifa kituo cha polisi  ili  waweze kuchukuliwa hatua haraka  ambapo amesesistiza  kwamba (UKAWA) wanataka  taarifa hiyo iwasilishwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa Jumatatu .
 
ITV imemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa dodoma  David Misime  na katibu wa bunge Dr.Thomas Kashilillah ambao  wamesema nao wanazisikia  taarifa hizo na wanazifanyia kazi ili kutoa taarifa yao.
 
source ITV
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger