".SERIKALI IACHE KUCHEZEA MAISHA YA WATANZANIA"WARAKA MUHIMU KWA WANANCHI WOTE KUTOKA KWA Prof IBRAHIM LIPUMBA KUPITIA KWA VYOMBO VYA HABARI

WARAKA MUHIMU KWA WANANCHI WOTE KUTOKA KWA Prof IBRAHIM LIPUMBA

KUPITIA KWA VYOMBO VYA HABARI

.SERIKALI IACHE KUCHEZEA MAISHA YA WATANZANIA
Hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati na hospitali za serikali inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya kushindwa kwa vituo vya huduma za afya kununua dawa Bohari la Dawa (MSD) kutokana na malimbikizo ya madeni. Kufikia Septemba 2014 deni ambalo Bohari la Dawa linadai hospitali na vituo vya serikali limekua na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 102. Mwishoni mwa mwaka 2013 deni hilo lilikuwa shilingi bilioni 76.4.
Bohari la Dawa litashindwa kabisa kununa dawa kwa sababu ya deni kubwa inalodiwa na makampuni yanayouza dawa kwenye bohari hilo.
Sera ya serikali ni vituo vya afya vya serikali kuwapa matibabu bure kina mama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano, wazee, watu wenye magonjwa sugu, watu wasiojiweza pamoja na watu wenye ulemavu. Kundi hili ni asilimia 75 ya wagonjwa wanaoenda kutafuta huduma katika vituo vya afya vya serikali.
Inasikitisha na inaonesha namna serikali ya CCM isivyomjali mwananchi wa kawaida, Waziri wa Afya anapozitaka hospitali kulipa madeni ya bohari la dawa kwa kutumia nusu ya fedha za uchangiaji zinazolipwa na wananchi. Hii ni sawa na kuzieleza hospitali hizo zisitoe huduma bila malipo kwani robo tatu ya wagonjwa wake ni wale ambao serikali imeeleza wape huduma bila malipo. Serikali imewafungia ngulai kina mama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano, wazee, watu wenye magonjwa sugu, watu wasiojiweza pamoja na watu wenye ulemavu kwa kuwaeleza kuwa watatibiwa bure. Wengi wao hawapati huduma bila malipo.
Vyombo vya habari vimemnukuu Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Mwigulu Nchemba akisema kuwa kiasi cha fedha zilizotolewa kwa ajili ya dawa katika mwaka 2013/14 ilikuwa shilingi bilioni 47 lakini ni shilingi bilioni 7 tu ndizo zilitumika katika kununua dawa. Hata hivyo serikali imeshindwa kueleza kwa nini kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha hizi. Shilingi bilioni 40 zimekwenda wapi?
Wakati wananchi wa kawaida wanakufa kwa kukosa dawa, serikali imeendelea kutumia mabilioni ya fedha kuchakachua maoni ya wananchi katika Bunge Maalum la Katiba. Ikulu imepanga kutumia bilioni 2.5 kuipigia kampeni Katiba Inayopendekezwa kupitia vyombo vya habari. Rais anaendelea kutumia mabilioni ya shilingi kufanya ziara zisizokwisha nchi za nje. Vigogo wa serikali na CCM wanaenda kutibiwa nje ya nchi. CCM haina huruma na mwananchi wa kawaida.
UFISADI WA IPTL UNATISHA
Wakati Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu, Serikali ya CCM imewawekea fursa wapambe wake kujichotea fedha za umma kupitia fedha zilizowekwa katika akaunti maalum ya Escrow kwenye Benki Kuu ya Tanzania. Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa baada ya Shirika la kufua na kusambaza umeme la Tanzania TANESCO kudai kuwa kampuni binafsi ya kufua umeme ya IPTL imekuwa inaitapeli TANESCO kwa kuitoza Capacity Charge kubwa kuliko makubaliano yaliyoko katika mkataba. Toka imeanzishwa kampuni ya IPTL imekuwa mzigo mzito kwa TANESCO na watumiaji umeme wa Tanzania kwa sababu ya kuilipa capacity charge kubwa na mashine zake zinatumia mafuta mazito kufua umeme. Mafuta mazito yana bei kubwa zaidi ya mara mbili ya gharama za gesi.
Kama viongozi wa serikali na TANESCO wangekuwa makini ingewezekana kabisa mitambo ya IPTL kuwa mali ya TANESCO mwaka huu wa 2014 kwani mkataba kati ya TANESCO na IPTL wa mwaka 1994 ulikuwa wa miaka 20 na baada ya hapo mitambo hiyo iwe mali ya TANESCO. Isitoshe kampuni ya Mechmar Corporation ya Malaysia ambayo ndiyo iliyoanzisha IPTL ilifilisika mwaka 2008. Kwa kuwa kulikuwa na madai ya Mechmar na IPTL kuidanganya TANESCO na kampuni hiyo kuwa imefilisika viongozi wa serikali na wanasheria wazalendo wangeweza kujikwamua kutoka jinamizi na gharama kubwa za IPTL.
Badala yake viongozi wa serikaliambao hawana hata chembe ya uzalendo kwa kushirikiana na matapeli wakaamua kuchota dola milioni 122 za Escrow Account na kuzikabidhi kwa kampuni ya kitapeli iliyodai kuinunua IPTL. Kampuni ya VIP Engineering and Management iliyokuwa mbia wa Mechmar Corporation ambayo haikuwekeza hata senti moja imelipwa dola milioni 70. James Rugemalira mmiliki wa VIP Engineering and Management amekaririwa kuyaita malipo hayo ni “vijipesa vya ugoro.”
Mwanasheria Mkuu wa serikali amenukuliwa akieleza kuwa fedha hizo siyo za umma wakati taarifa ya fedha ya TANESCO inaonesha kuwa ni fedha za akiba (Reserve Funds). Inaaminika kuwa kuna fedha nyingine - dola milioni 128 katika Tegeta Escrow Account ambazo zitachukuliwa na kampuni ya kitapeli iliyonunua IPTL.
Viongozi wa serikali kushiriki kuihujumu TANESCO kunaonesha jinsi CCM kimekuwa Chama Cha Mafisadi kisichokuwa na hata chembe ndogo ya uzalendo.
Tunaisubiri kwa hamu taarifa ya ukaguzi ya CAG ya Tegeta Escrow Account. Ni matumaini yetu CAG ameifanya kazi hii kwa uadilifu na weledi wa juu bila woga na ataeleza ukweli wa ufisadi huu. Waliofisidi na walioruhusu TANESCO iibiwe wawajibike na wachukuliwe hatua za kisheria.
CHANGAMOTO KWA SERIKALI IJAYO YA UKAWA
Serikali ijayo itakuwa na changamoto kubwa. Pamoja na kutokuwepo Katiba ya Wananchi, itarithi serikali yenye malimbikizo makubwa ya madeni ya nje na ndani, matumizi mabaya ya fedha za umma na ukosefu mkubwa wa uadilifu na uwajibikaji. Pamoja na kuainisha sera zetu, wataalam wetu wanapitia kwa umakini uchambuzi wa matumizi ya fedha za umma, Public Expenditure Review na taarifa za CAG kubaini vizuri maeneo muhimu ya kusimamia ili kuokoa fedha za umma zinazotumiwa vibaya na kuziweka katika maeneo muhimu ya kuwapa wananchi huduma bora za afya, kuboresha elimu kwa watoto na vijana wetu, kujenga miundombinu imara, kuimarisha kilimo na kukuza uchumi unaoongeza ajira. Kwa miaka 10 ijayo Tanzania inaweza kukuza uchumi kwa wastani wa asilimia 10 unao ingeza ajira kwa wingi kwa vijana wetu. Haya yanawezekana ikiwa tutakuwa na uzalendo wa dhati na kuweka mbele maslahi ya wananchi wa kawaida na kutumia raslimali na maliasili ya nchi kuleta neema kwa wananchi wote.
HAKI SAWA KWA WOTE
Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti,
Jumapili, 09 Novemba 2014.

Share this article :

Post a Comment

Support : Creating Website | Jordan Digital |
Copyright © 2011. MAWIO HALISI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by jordan digital
Proudly powered by Blogger